KANUNI NNE (4) ZA KIROHO


Kila jambo maishani lina kanuni zake. Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushirikiana na Mungu.

1. MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.

UPENDO WA MUNGU 
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16

MPANGO WA MUNGU KWAKO
Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10

Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo?
Ni kwa sababu . . .

2. MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na Mungu.Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.

MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI

Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.Warumi 3:23

Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.

MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU

Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu. Isaya 59:2

Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.

Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .

3. YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.

ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU

Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18

YESU YU HAI

Kristo alikufa kwa ojili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho 15:3,4

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:6

Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.

Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .

4. INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.Yohana 1:12

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9

INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO

Tazama, nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .

Kumpokea Yesu Kristo ni:

Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa.Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyopenda.

Je, ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano wa maisha yako?

Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?

UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA

Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.

Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.

Je, sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?

Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.

YESU YUMO MAISHANI MWAKO

Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.

ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE

Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwana. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu. 1 Yohana 5:11-13

Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.

USIYATEGEMEE MAWAZO YA MOYO WAKO.

Unaweza kujisikia leo unalfuraha kisha kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. Waebrania 13:8.

Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.Tunapotii ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni) huongozwa vyema.Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hali ya kujisikia ya moyo.

Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.

Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.

KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU

Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.

Yesu ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)Umesamehewa dhambi zako. (Wakolosai 1:14)Umefanyika kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)

Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?

Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.

Tuombe tukiwa huru.

Na sasa je?

JINSI YA KUKUA KIROHO

Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:

Zungumza na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7)Soma Neno la Mungu (Matendo 17:11)Uwe mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21)Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)

NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA

Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)

Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.

Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.

Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.

Share:

Maisha na neno la MUNGU

TAMBUA NYAKATI ZA MWISHO
1Timotheo 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Share:

SOMO: KUVUKA NG’AMBO YA PILI..... na ASKOFU: CHALRES KARIUKI – KENYA


SOMO: KUVUKA NG’AMBO YA PILI
Baada ya Yesu kuhubiri kukawa usiku, akauacha mkutano na kuwaambia wanafunzi wake wavuke ng’ambo. Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.”Kule ng’ambo kuna vitu vikubwa sana.
Share:

Huwezi kusimama kinyume na ibilisi bila NGUVU ya Mungu.....Mtume na Nabii: Josephat Elias Mwingira

.Mtume na Nabii: Josephat Elias Mwingira

Huwezi kusimama kinyume na ibilisi bila NGUVU ya Mungu. Unaweza kuona watu waliokoka kama ni watu waliopoteza muelekeo, ambao wamejaa na matatizo na mahangaiko ya kila aina, lakini hiyo si kweli, ukweli wa mambo ni kuwa watu waliiokoka ni washindi. Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. ”
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU 6.... na Mwl Christopher Mwakasege,



                                                    SURA YA SITA

        UMUHIMU WA KUWEKA IMANI YAKO KATIKA
                                JINA LA YESU KRISTO        
     
“Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa Na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango WA hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.”  (matendo ya mitume 3:1-8)
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU 5.... na Mwl Christopher Mwakasege,

    SURA YA TANO

OMBA KWA JINA LA YESU KRISTO

KILA mkristo anapenda awe na maisha ya maombi yaliyo na mafanikio – anapenda akiomba kitu kwa Mungu ajibiwe. Lakini mara nyingi nimewasikia wakristo kadhaa wakisema wameomba jambo Fulani kwa Mungu lakini hawajajibiwa. Wengine wanapofikia hali ya namna hii, hukata tama – hata wokovu unaanza kupoa utamu wake.
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU 4.... na Mwl Christopher Mwakasege,

    SURA YA NNE

                        MAMLAKA ULIYONAYO UNAPOLITUMIA JINA LA YESU KRISTO!

      Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.”  (Wafilipi  2:9-11)
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU 3.... na Mwl Christopher Mwakasege,

  SURA YA TATU
YESU KRISTO – JINA LA MWANA WA MUNGU

Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa galilaya, unaoitwa nazarethi, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu aliyeitwa Yusufu. Malaika Gabriel alipofika nyumbani kwa mariamu alimpa ujumbe wa Mingu yakiwemo maneno haya;
      “Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:31-33).
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU 2.... na Mwl Christopher Mwakasege,

   SURA YA PILI

                     NGUVU UNAYOPATA UNAPOTAFAKARI JUU YA JINA LA YESU KRISTO
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana” yoshua 1:8
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU 1.... na Mwl Christopher Mwakasege,

        Sura ya Kwanza

                      JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFLME WA MBINGUNI.
“Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; Na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; Na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.” (mathayo 16:16-18)
Share:

UWEZA WA JINA LA YESU... na Mwl Christopher Mwakasege,

Utangulizi


UWEZA WA JINA LA YESU

Mtume Paulo anasema katika Waraka wake kwa Wakolosai sura ya tatu na mstari wa kumi na saba kuwa; “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”
Share:

BABA YUPO NASI

BABA YUPO NASI

Popular Posts

Search This Blog

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages