YESU KRISTO – JINA LA MWANA WA MUNGU
Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa galilaya, unaoitwa nazarethi, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu aliyeitwa Yusufu. Malaika Gabriel alipofika nyumbani kwa mariamu alimpa ujumbe wa Mingu yakiwemo maneno haya;
“Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:31-33).
Yusufu alipoona ya kuwa mariamu lalikuwa na mimba, aliazimia moyoni mwake kumwacha kwa siri. Lakini akiwa katika kuwaza hayo, malaika wa bwana alimtokea katika ndoto, akisema;
“Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” (Mathayo 1:20-21)
Je! Umewahi kujiuliza kwa nini Yusufu na mariamu waliambiwa ya kuwa mtoto huyo atakayezaliwa jina lake wamwite Yesu! Je hili jina lilitoka wapi? Je! Yusufu na mariamu wangeamua kupuuza maneno ya malaika wa Mungu na kumpa motto jina jingine kungetokea nini? Hebu tafakari juu ya maswali haya, yatakusaidia kuchochea kiu ya kutaka kujua siri iliyomo ndani ya jina hili la ajabu.
Yesu Kristo alipewa hili jina pamoja nasababu mbalimbali zilizotolewa zilikuwemo hizi mbili kubwa zifuatazo:
1. Ni mrithi
Imeandikwa hivi:
“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.” (Waebrania 1:1-4)
Kwa mistari hii ya mwanzo ya waraka wa waebrania tunaona ya kuwa Yesu Kristoamewekwa na Mungu Baba yake “kuwa mrithi wa yote”. Na katika mambo aliyopewa kuyarithi ni pamoja na JINA HILI LA YESU – NDIYO maana imeandikwa “amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao” (waebrania 1:4)
Kwa hiyo ni wazi kwamba huyu mwana wa Mungu alipewa jina hili la Yesu kwa kuwa yeye MRITHI WA YOTE ya Baba yetu mungu aliye mbinguni. Siku moja nilipokuwa nikifanya sala ya asubuhi ofisinikwangu miaka michache iliyopita, Roho mtakatifu aliniuliza ndani ya roho yangu swali hili, “Je! Jina la Baba yako aliye mbinguni ni lipi?”
Mara moja nikakumbuka kuwa sijawahi kulikumbuka jambo hili, ingawa mara kwa mara naisema sala ya Bwana inayoanza na baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe…” Je! Ni jina lipi hilo ninalosema litukuzwe?
Pia, nakumbuka ya kuwa Yesu Kristo siku ile alipofufuka, alimwambia mariamu magdalenakuwa, “Yesu akamwambia. Usinishike; Kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu” (yohana 20:17)
Kwa manenohaya ninaelewa ya kuwa Baba yake Yesu Kristo ni Baba yangu pia kwa kuwa nimo ndani yake. Ikiwa Mungu ni Baba yangu aliye nizaa mara ya pili kwa Roho wake mtakatifu, basi inashangaza kuona kuwa nilikuwa silifahamu jina la Baba yangu mzazi wa kiroho.
Hebu fikiria ningeulizwa jina la mzazi wangu kimwili halafu niseme silifahamu, si watu wangenishangaa? Wangejua hakika yakuwa sina uhusiano wa karibu na mzazi wangu! Niliona ni muhimu nilifahamu jina la Baba yangu aliye mbinguni. Nikaanza kulitafakari upya neno la Mungu ili niweze kupata jibu la jambo hili.
Baada ya maombi ya siku nyingi na muda mwingi wa kulisoma neno la Mungu, Roho mtakatifu alinionyesha ya kuwa katika kipindi hiki cha agano jipya Mungu amejifunua kwetu katika Jina la Yesu Kristo. Kwa maneno mengine jina la Baba yetu aliye mbinguni ambaye pia ni baba wa Yesu Kristo ni YESU.
Unaweza ukawa unajiuliza inakuwaje jambo hili. Lakini kabla ya kuendelea kusita, nadhani utakubaliana na mimi ya kuwa mtu hawezi kurithi kitu chake, bali anarithi kitu kisicho chake. Pia, mtu hawezi kurithi Jina Lake, bali anarithi jina lisili lake. Kwa hiyo biblia inapotuambia ya kuwa Baba amempa Mwana wake urithi wa Jina lake, ina maana ya kuwa hapo mwanzo jina la Yesu lilikuwa ni la Mungu Baba hadi alipoamua kumpa jina hilo motto wake kama sehemu ya urithi wake! Ndiyo maana yesu Kristo alisema, “
Kwa maneno mengine alitaka tujue ya kuwa jina la Yesu Kristo si “jina lake mwenyewe.” Lingekuwa “jina lake mwenyewe” angepokelewa, lakini kwa kuwa jina la Yesu Kristo alilokuja nalo ulimwenguni ni “jina la Baba yake” hawakumpokea.
Nadhani sasa unaweza ukaelewa kwa nini ina hili la Yesu Kristo linaitwa ni jina lipitalo majianyote mbinguni, duniani na hata chini ya nchi (wafilii 2:9-10). Jina la Yesu Kristo ni jina lipitalo kila jina kwa kuwa ndilo jina la Mungu Baba pia. Mungu Baba angekuwa na jina jingine kuliko hili, biblia isingesema hata mbinguni jina la Yesu Kristo liko juu ya majina yote.
Kwa hiyo jina la Yesu Kristo ni la Mungu Baba ambalo amempa mwana wakewa pekee ili ajulikane kwa hilo. Ndiyo maana tunasema Yesu Krsto ni jina la mwana wa Mungu alilorithi toka kwa Baba yake. Naamini kuwa sasa utaelewa Yesu Kristo alikuwa ana maana gani alipokuwa akituombea kwa Baba yake katika sala iliyoandikwa katika kitabu cha Yohana sura ya kumi na saba aliposema,
“….Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu…Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, Kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, Mimi naliwalinda Kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza….Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo….” (Yohana 17:6,11,12,26)
Yesu Kristo anamwambia Baba yake katika maombi ya kuwa JINA LAKE ALILOMPA ametujulisha, amelidhihisha kwetu, ametulinda na kututunza nalo – Ni jina gani hilo kama si jina hili la Yesu Kristo! Kwa kuujua undani huu tunajua hakika ya kuwa katiaka jina hili la mwana wa Mungu _ jina la Yesu Kristo kuna uweza wa kifalme, ushauri wa ajabu, uungu wenye nguvu, Ubaba wa milele, na ufalme wa amani wa Mungu baba!
2. Ni mtii
Kitabu cha wafilipi 2:9,11 kinasema hivi,
“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Hii sentensi inayosema, “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina”; inatuonyesha ya kuwa ‘Kwa hiyo tena Mungu’ aliamua kumpa mtoto wake jina lipitalo kila jina; jina la Yesu kwa kuwa motto wake alifanya jambo Fulani lililompendeza.
Jambo hili ni lipi? Ni UTII – alikuwa mtii hata mauti; naam, mauti ya msalaba.
Imeandikwa hivi, “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba” wafilipi 2:5-8)
Mungu Baba alipoona ya kuwa mwana wakewa pekee amekuwa mtii katika yote aliyomwagiza hata mauti, naam, mauti ya msalaba, ili watu wote wanaomwamini waokolewe, aliamua kumkirimia jina lile lipitalo kila jina - jina la Yesu!
Ndiyo maana Yesu Kristo alikuwa na ujasri wa kuyasema maneno yafuatayo:
“Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana WA Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa Mimi ndiye; Na ya kuwa SIFANYI NENO KWA NAFSI YANGU, ila kama Baba alivyonifundisha NDIVYO NINENAVYO. Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu NAFANYA SIKUZOTE YALE YAMPENDEZAYO”
Maisha ya Yesu Kristo hapa ulimwenguni yalikuwa ni maisha ya utii – alisema tu yale ambayo aliyasikia kwa Baba yake. Pia, alifanya siku zote yale yampendezayo Baba yake. Kwa sababu hiyo Baba yake alikuwa pamoja naye kwa njia ya Jina la Yesu kila mahali alipokuwa.
Jina la Yesu Kristo tumepewa na sisi pia.
“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye” (wafilipi 8:16-17)
Mtu aliyezaliwa mara ya pili au kwa lugha nyingine mtu aliyeokoka kwa uwezo wa Roho mtakatifu anafanyika mwana wa Mungu. Kwa kufanyika kuwa mtoto wa Mungu, anakuwa mrithi wa Mungu. Kumbuka kuwa Kristo ni mrithi wa Mungu, na kati ya mambo aliyoirithi ni jina la Yesu. Biblia inatuambia kuwa kila aliye mwana wa Mungu ni mrithi pamoja na Kristo wa mambo ya Mungu aliye Baba yetu.
Kumbuka kuwa tu warithi pamoja na Kristo ina maana ya kuwa tumeshirikishwa urithi huu ndani yake Kristo. Kwa kuwa tu warithi pamoja na Kristo ina maana ya kuwa sisi tumepewa jina la Yesu! Ni halali yetu kulitumia sawasawa na neno la Mungu linavyotuagiza. Jina la Yesu Kristo ni urithi wetu pia!
Ndiyo maana kati ya maagizo aliyitupa Yesu Kristo alisema, “ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” (marko 16:17-18)
Kwa hiyo ukitaka kulitumia Jina la Yesu Kristoo kihalali na uweze kuona uwezo na mamlaka yake ni muhimu kwanza, uwe mwana wa Mungu kwa kumpokea Kristo moyoni mwako kama Bwana na mwokozi wako; pili, uwe mtii ukifuata maagizo ya neno la Mungu katika Roho mtakatifu.
No comments:
Post a Comment